Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Homera: Watakaotumia vibaya fedha za lishe kushughulikiwa

HOMERA Watakaotumia vibaya fedha za lishe kushughulikiwa

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amewataka viongozi wa Halmashauri zote za mkoa huo kumpatia taarifa za watumishi watakaotumia fedha za lishe kinyume na maelekezo ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera ametoa kauli hiyo wakati wa zoezi la utiaji saini wa mkataba wa afua za lishe ambao una lengo la kutoa elimu kwa wananchi ili kukabiliana na tatizo la udumavu uliosainiwa na  wakurugenzi na wakuu wa Wilaya.

Mratibu wa lishe  Mkoa wa Mbeya, Benson Sanga amesema mkoa umetenga kiasi cha sh. milioni 400 kutekeleza afua mbalimbali za lishe katika kipindi cha mwaka 2022 huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Ezekiel Maghehema akielezea utekelezaji huo.  

Chanzo: www.tanzaniaweb.live