Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hofu ya upungufu wa chakula mikoa 13

67681 Pic+njaa

Mon, 22 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Tathmini ya hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula kwa misimu miwili mfululizo imebainisha dalili za upungufu wa chakula katika mikoa 13 na halmashauri 46.

Tathmini hiyo ya mwaka 2018/19 na 2019/20 iliyofanywa na Wizara ya Kilimo Mei na Juni, inaonyesha uwezekano wa kuwepo upungufu huo katika halmashauri za Chamwino, Chemba, Kondoa, Kongwa na Mpwapwa mkoani Dodoma.

Nyingine ni Halmashauri ya Bunda DC, Bunda TC, Musoma DC, Musoma MC na Rorya mkoani Mara, Uyuyi, Igunga, Nzega DC, Nzega TC na Kaliua (Tabora) na Kishapu, Shinyanga DC, Shinyanga MC na Msalala (Shinyanga).

Pia upungufu huo unaweza kutokea Mwanga, Same, Siha na Hai (Kilimanjaro), Misungwi, Ukerewe, Kwimba na Sengerema (Mwanza), Manyara, Simanjiro, Kiteto, Hanang na Mbulu TC (Manyara), Itilima, Maswa, Meatu na Busega (Simiyu), Longido, Ngorongoro na Monduli (Arusha), na Ikungi, Manyoni na Singida DC (Singida).

Halmashauri nyingine ni Tanga Jiji (Tanga), Lindi (Lindi) na Iringa (Iringa).

Kwa habari zaidi soma gazeti la Mwananchi la leo Jumapili Julai 21, 2019

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz