Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hofu ya corona yamfanya ajifungie ndani miezi mitano sasa

HOFU.jpeg Hofu ya corona yamfanya ajifungie ndani miezi mitano sasa

Fri, 29 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KATIKA kipindi hiki ambapo Dunia imekuwa ikiathiriwa na mlipuko wa homa kali ya mapafu

inayosasababishwa na virusi vya corona (Covid-19), hofu kubwa imetanda kwa watu ambao tayari wanamagonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Hii inatokana na uthibitisho wa wataalamu wa afya kusema kwamba virusi vya corona vina nafasi kubwa zaidi kumshambulia na kumwathiri mtu ambaye kinga zake za mwili ni dhaifu.

Moja ya kundi ambalo liko hatarini zaidi endapo watapata virusi vya corona ni wagonjwa wanaoungua ugonjwa wa lupus, hii ni kwa sababu tayari kinga zao ziko katika mfumo wa to- fauti.

Lupus ni ugonjwa unaotokea pale ambapo kinga za mwili huacha kazi yake ya kulinda mwili na badala yake kushambulia kwa kuonesha uharibifu katika sehemu mbalimbali za mwili kama ngozi, figo na mapafu.

Ugonjwa huu pia unatabia ya kujificha kwenye magonjwa mengine hasa unaposhambulia mapafu, huweza kudhaniwa kama Kifua Kikuu (TB), hali hiyo husababisha wagonjwa hao kupewa dawa za TB.

Ni rahisi zaidi wagonjwa hawa kupata maambukizi ya ma- gonjwa mengine, hii ni kutokana na miili yao kutokuwa na kinga ya kutosha.

Kwa mujibu Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Dk. Francis Furia, lupus ni ugonjwa unaoshambulia zaidi watu weusi hasa wanawake.

Dk. Furia ambaye pia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto na Figo, anasema ni muhimu wagonjwa wa lupus kujilinda wakati wote kutokana na urahisi wa kupata maambukizi.

“Kama tunavyojua, kwa kawaida kazi ya jeshi ni kuilinda nchi ili maadui wasiivamie pale ambapo jeshi linapoacha kazi yake ya kuilinda nchi na kuanza kuishambulia, hii ndio maana halisi ya ugonjwa wa lupus.

“Huu ni ugonjwa unaoshambulia sehemu mabalimbali za mwili, ndio maana unaitwa ‘systematic Erythematosus disease’ unatokea baada ya kinga za mwili kuanza kushambulia mwili, kama tunavyojua kazi ya

kinga za mwili ni ulinzi lakini zinapogeuza kazi zake huwa hatari,” anaeleza Dk. Furia.

Anasema hakuna utafiti wa kisanyasi unazothibitisha sababu za hali hiyo kutokea.

“Utafiti unasema ugonjwa huo unawaathiri zaidi watu weusi hasa barani Afrika, ukienda nchi za Ulaya wanaopata pia ni watu weusi.

“Asilimia kubwa ya wanaoathirika ni wanawake, katika kila watu 20 anayepata ni mwanaume mmoja, huku idadi ya watu wazima ikiwa kubwa zaidi kuliko watoto.

“Tafiti bado zinaendelea kufanyika kubaini chanzo cha ugonjwa huo ila inahusishwa pia na miale ya jua, hali ya hewa lakini hakuna uthibitisho wa hilo hata vinasaba vinahusishwa pia,” anabainisha Dk. Furia.

Anasema kuwa utafiti wa Muhimbili wa kuanzia mwaka 2012 hadi 2018 ni watoto wanne pekee waliopatikana na ugonjwa huo.

Hivyo, hayo ni magonjwa yanayotokea kwa watu wachache huku tafiti za kidunia zikinaonesha kwamba kuna wagonjwa 20 hadi 150 kwa kila watu 100,000.

CORONA YAMUWEKA NDANI MIEZI MITANO

Hajrrath Mohammed, ni msichana mwenye umri wa miaka 25 anayesumbuliwa na ugonjwa wa lupus, anasimulia jinsi ambavyo mlipuko wa ugonjwa wa corona ulivyobadilisha maisha yake.

Hajrrath anasema ni miezi mitano sasa hajatoka nje ya nyumba yao tangu ugonjwa wa corona kuanza kuripotiwa na kutajwa kuongezeka kwa kasi duniani.

Sababu kubwa inayomfanya kukaa ndani ni hofu ya kuweza kuambukizwa virusi hivyo.

Anasema amekuwa akikaa katika chumba chake ambapo mtu yeyote hawezi kuruhusiwa kuingia isipokuwa anayechukua tahadhari za kiafya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live