Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiki ndio kijiji kisicho na viongozi wa serikali ya kijiji Njombe

Picha Kijiji Data Hiki ndio kijiji kisicho na viongozi wa serikali ya kijiji Njombe

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wananchi wa kijiji cha Mawande kilichopo kata ya Utengule katika halmashauri ya mji wa Makambako wamelalamikia kukosekana kwa mtendaji na mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho na kueleza kuwa hali hiyo imesababisha kusimama kwa shughuli za kimaendeleo.

Wakizungumza mbele ya kamati ya siasa ya wilaya ya Njombe, Wananchi hao wamesema wanashangazwa na kitendo cha mwenyekiti wa kijiji hicho kusimamishwa kutekeleza majuku yake na viongozi wa chama cha mapinduzi kata,na kuitaka serikali kutatua changamoto hiyo kwani inakwamisha shughuli za kimaendeleo ikiwemo ujenzi wa shule shikizi ya msingi.

Wananchi hao,Baraka Fifi,Milton Kiwovele,Josphat Kilasi na Christopher Mhema wameiomba serikali kutatua changamoto ya mpaka katika kijiji hicho huku wengine wakilalamikia changamoto ya barabara na umeme.

Afisa mtendaji kata ya Utengule Moses Mwalongo amekiri kuwepo kwa changamoto ya kukosekana kwa watendaji wa vijiji viwili ikiwemo Ngamanga na Mawande.

Naye Diwani wa kata ya utengule Stephano Mgoba amesema mpaka sasa mtendaji wa kukaimu nafasi katika kijiji cha Mawande amepatikana na kueleza kuwa kamati ya siasa kata ndiyo imehusika kumsimamisha mwenyekiti wa kijiji hicho kutokana na hali yake ya kiafya kutokuwa sawa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Njombe Justin Nusulupila ameahidi kurudi katika kijiji hicho ili kuona namna ya kumaliza mgogoro huo uliopo ambao umesababisha mwenyekiti kuondolewa katika nafasi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live