Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hiace kuondolewa katikati ya Jiji la Mwanza

31917 Mwanza+pic Mwanza

Mon, 17 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Huenda habari hii isiwe nzuri kwa wamiliki na madereva wa Hiace zinazotoa huduma ya usafiri jijini Mwanza baada ya Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kujipanga kuziondoa ili kupunguza msongamano wa magari.

Hiace zenye uwezo wa kupakia abiria 16 zitaondolewa na kuanza kutoa safari nje ya Jiji hilo kupisha daladala zinazopakia abiria 25 hadi 40 kwa wakati mmoja.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili Desemba 16, 2018 ofisa mfawidhi wa Sumatra mkoani Mwanza, Gabriel Anthony amesema, “tulishatoa muda wa kutosha. Zoezi hilo limeanza tangu Agosti 2018 na litafikia ukomo Oktoba 2019. Yeyote atakayekiuka atachukuliwa hatua stahiki.”

Amesema Hiace zitakuwa zikitoa huduma ya usafiri nje ya Jiji la Mwanza na tayari wameanza kutoa leseni za daladala kufanya safari katika maeneo ya Kisesa-Kishiri hadi Nyashishi na Uwanja wa Ndege-Ilemela hadi Kisesa.

Baadhi ya wamiliki wa Hiace hizo wamesema hatua hiyo itapunguza kipato chao.

“Mimi ningeulizwa kutoa maoni kuhusu hili ningekataa maana huduma ya magari makubwa kama vile Tata na Coaster ni sawa na hii tunayotoa sisi na nauli, safari na mfumo wa uendeshaji ni ule ule,” amesema, Robert Mushi, mmiliki wa Hiace.

Naye Jeremia Amos amesema Hiace hizo zimetoa ajira nyingi, hasa kwa vijana hivyo kuziondoa katikati ya Jiji kutasababisha wengi kuziuza na kuyaegesha majumbani mwao.

 

 



Chanzo: mwananchi.co.tz