Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hi kali! Form 1 waripoti shuleni watano kati ya 59

Watano Kati Ya 59 Form One Hi kali! Form 1 waripoti shuleni watano kati ya 59

Wed, 10 Jan 2024 Chanzo: Millard

Wakati Wanafunzi wa Shule za Sekondari na Msingi wakianza masomo kwa siku ya pili leo nchini kote kwa muhula wa mwaka 2024, hali imekua tofauti kwa shule ya Sekondari Parakuyo iliyopo Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro baada ya Wanafunzi watano pekee wote wakiwa ni Wavulana kuripoti kati ya Wanafunzi 59 waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika Shule hiyo ya Kata.

Hayo yamejiri baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka @shakazulu36 kutembelea Shule hiyo ambapo zaidi ya asilimia 95 ya Wananchi wanaoshi katika eneo hilo ni Wafugaji Jamii ya Kimasai na kukuta hali ya kuzorota kuripoti kwa Wanafunzi, imeelezwa kuwa licha ya Shule hiyo kuwa ya kutwa, Wasichana huishi Hostel zilizopo Shuleni hapo na Wavulana hutokea nyumbani.

DC Shaka anatoa maagizo Kwa Viongozi wa Kata hiyo kuhakikisha wanawatafuta popote walipo Wanafunzi hao 54 ambao hawajaripoti hadi sasa ili waanze masomo.

Jumla ya Wanafunzi 59 wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Shuleni hapo wakiwemo Wavulana 30 na Wasichana 29.

Chanzo: Millard