Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Helkopta yatumika kudhibiti tembo Same

Helkopta Sa Helkopta yatumika kudhibiti tembo Same

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imetumia Helikopta kutafuta makundi ya Tembo waliozagaa katika Vijiji 25 vya Wilaya ya Same na kuwavisha vifaa maalum vya mawasiliano kufuatilia mwenendo wao ili kudhibiti Wanyama hao kuvamia Makazi ya Watu na kuharibu shughuli za kibinaadamu na uhifadhi.

Zoezi hili limefanyika kutekeleza agizo la Waziri wa Maliasili na Utalii Mohammed Mchengerwa alilolitoa hivi karibuni alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Same na kuiagiza TANAPA kupeleka Helikopta kuondoa makundi hayo ya Tembo na kuwarudisha hifadhini.

Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni ameshukuru na kupongeza jitihada hizo za Wizara pamoja na uharaka wa kutekeleza ahadi hiyo kuwawezesha Wananchi kuendelea na shughuli zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live