Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hela ya mkaa ilivyokatisha uhai wa mfanyabiashara

Mkaa Dar Matumizi Hela ya mkaa ilivyokatisha uhai wa mfanyabiashara

Fri, 24 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara wa mkaa Abdalah Chenya mkazi wa Miswe, Kibaha mkoani wa Pwani amepoteza uhai kwa madai ya kupigwa na bunduki na msimamizi wa kituo cha kukusanya ushuru wa bidhaa hiyo kituo cha Ruvu Darajani.

Chenya ambaye ni marehemu alikutwa na mauti Februari 20, 2023 saa moja jioni wakati akiwa kituoni hapo akiwa na pikipiki ambayo huwa anaitumia kusafirishia bidhaa hiyo kutoka vijijini na kwenda kuuza mjini.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Pius Lutumo mfanyabiashara huyo akifika kituoni hapo akawa anadaiwa pesa ya kulipia ushuru wa halmashauri lakini kwa hali ya tofauti kukawa na ugumu kwake kutekeleza hilo na badala yake aliwapigia simu wafanyabishara wenzake Ili waje kumsaidia kukomboa pikipiki hiyo iliyokuwa na mkaa.

"Alifika akawa anadaiwa ushuru lakini aliwapigia simu wenzake waje wamsaidie kukomboa pikipiki na walifika wakiwa na silaha za jadi wakachukua kwa nguvu pikipiki hiyo wakaanza kuondoka nayo," amesema.

Amesema kuwa kabla hawajifika mbali wauza mkaa hao walimrudia msimamizi huyo wa kituo cha ushuru cha halmashauri na kumtolea maneno kuwa bunduki aliyonayo ni toyo na haiwezi kufanya lolote huku wakitaka kumpora silaha hiyo aina ya gobole.

"Walianza kutaka kumpora sasa huyo msimamizi wa kituo hicho alifikia uamuzi wa kufyatua lisasi na ndipo ilimfikia huyo mfanyabiashara na kumjeruhi," amesema.

Amesema kuwa baadaye ilibainika kuwa muuza mkaa hiyo alipoteza maisha, mbapo baada ya taratibu mbalimbàli mwili wake ulikabidhiwa kwa ndugu na kusafirishwa mkoani Singida kwaajili ya mazishi.

Kwa siku za karibuni Wafanyabiashara wa mkaa hasa wanaosafirisha bidhaa hiyo kutumia pikipiki wamepungua ikilinganishwa na wakati wa nyuma ambapo walikuwa wengi barabarani wakitokea Vijijini kupeleka bidhaa hiyo mjini.

Taarifa zinaeleza kuwa kupungua kwao kumetokana na mamlaka za kudhibiti sheria za misitu kuongeza doria za mara kwa mara maeneo mbalimbali ikiwemo vichochoroni na barabarani lengo likiwa ni kudhibiti ukataji holela wa miti unaoathiri mazingira.

Kwa mujibu wa takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na mamlaka mbalimbali, zinaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watumiaji wa Mkaa ni wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, huku wateja wanaowafikishia bidhaa hiyo ni kutoka mikoa ya jirani ikiwemo Pwani na kwamba baadhi yao wanakikuka taratibu za uvunaji endelevu wa mazao ya misitu jambo ambalo ni hatari kwa mazingira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live