Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Haya hapa majina 19 ya waliofariki kwa ajali ya ndege Bukoba

Vifo Bukoba Ndege Watu 19 ya waliofariki kwa ajali ya ndege Bukoba

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Kagera (RC), Albert Chalamila ametaja majina 19 ya watu waliopoteza maisha kufuatia ajali ya ndege ya Shirika la Precision Air iliyoangukia Ziwa Victoria mkoani humo asubuhi ya jana Jumapili, Novemba 6, 2022.

Chalamila ametaja majina hayo mbele ya waandishi wa habari ambao ni;

1. Atulinde Biteya

2. Aneth Biteya

3. Neema Faraja

4. Hanifa Hamza

5. Aneth Kaaya

6. Victor Laurean

7. Said Malat Lyangana

8. Iman Paul

9. Faraji Yusuph

10. Dk Boniface Jullu

11. Sauli Epimark

12. Zacharia Mlacha

13. Eunice Ndirangu

14. Mtani Njegere

15. Zaituni Shillah

16. Dr. Alice Simwinga

17. Buruani Bubaga – Rubani

18. Peter Odhiambo - first officer.

19. Mmoja ni sista hajatambulika jina lake

Ndege hiyo aina ya Air ATR 42 mali ya Precission Air ilikuwa ikitokea jijini Dar es Salaam kwenda Bukoba.

Mkuu huyo wa mkoa amesema tayari Waziri Mkuu Kassim Majaliwa yupo mkoani Kagera kuungana na wananchi wa mkoa kuaga miili ya watu waliopoteza maisha kufuati ajali hiyo akimwakilisha pia Rais Samia Suluhu Hassn.

Amesema ratiba ya misa ya kuaga miili ya wote waliopoteza maisha itaanza saa nne asubuhi katika Uwanja wa Kaitaba ambapo dua na sala zitaendeshwa na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo.

Mara baada ya kuwasili mkoani humo, Majaliwa amesema,”Rais Samia ameniagiza kuja kufuatilia zoezi hili na kuhakikisha linakwenda salama, pia ameguswa sana na tukio hili, na amekuwa akifuatilia kwa karibu ili kuhakikisha zoezi la uokoaji linafanyika kwa mafanikio.”

Majaliwa amesema abiria 26 wameokolewa na kukiwa na miili 19 ambayo imetolewa katika eneo la ajali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live