Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatma ya pori tengefu la Loliondo kujulikana karibuni

65696 Pic+loliondo

Sat, 6 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Serikali ya Tanzania inatarajia kutoa mwongozo hivi karibuni juu ya uhifadhi wa eneo la pori tengefu la Loliondo wilaya ya Ngorongoro mkoa wa Arusha ambalo limekuwa na migogoro tangu mwaka 1994.

Mkurugenzi wa wanyamapori wa wizara ya Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Dk Maurus Msuha ametoa taarifa hiyo leo Ijumaa Julai 5, 2019 katika mkutano wa mwaka wa wahariri na waandishi waandamizi ulioandaliwa na Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa).

"Serikali itatoa mwongozo juu ya kuhifadhi eneo la pori tengefu la Loliondo hivi karibuni ili kuhakikisha eneo hilo linaendelea kuhifadhiwa kwani ni muhimu sana katika kulinda ikolojia ya Serengeti," amesema.

Pori Tengefu la Loliondo limekuwa na migogoro baina ya wahifadhi na wafugaji wa vijiji vinavyozunguka pori hilo ambalo linapakana na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa mwaka 2018 aliunda kamati maalum ya kutafuta suluhu ya migogoro ya Loliondo ambayo tayari ilitoa mapendekezo kadhaa ikiwepo kuanzisha mamlaka ya kusimamia eneo hilo ama kuanzishwa hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Loliondo.

Chanzo: mwananchi.co.tz