Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatma ya mgomo wa daladala Mbeya Jumatano

Mgomo Mbeya Magari Magari.png Hatma ya mgomo wa daladala Mbeya Jumatano

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: mwanachidigital

Baada ya kikao cha zaidi ya masaa sita hatimaye Serikali imeamuru wamiliki wa mabasi kurejesha huduma ya usafiri jijini Mbeya hadi Jumatano itakapotolewa tamko rasmi kuhusu ongezeko la nauli.

Jana Oktoba 16 daladala jijini Mbeya zimegoma kutoa huduma na kusababisha adha ya usafiri kwa wananchi huku bajaji, pikipiki na gari binafsi zikitumika kutoa huduma hiyo.

Kufuatia adha hiyo, Serikali jijini hapa ilijifungia kwa muda wa takribani masaa saba pamoja na wamiliki wa vyombo hivyo ili kupata muafaka chini ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu baada ya kikao hicho, Ofisa Mfawidhi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (Latra) mkoani hapa, Omary Ayoub amesema wameomba huduma hiyo irejee.

Amesema pamoja na kurejesha huduma hiyo ya usafiri, wanatarajia kuwa na kikao cha wadau keshokutwa Jumatano kujadili nauli mpya akiwaomba wananchi kuwa watulivu.

“Malalamiko yao zaidi ilikuwa ni kuongeza nauli, lakini tumeowaomba waingize magari barabarani kwa siku hizi mbili ili Jumatano tuweze kuja na maazimio rasmi kwa kushirikisha wadau wakiwamo wananchi wenyewe,” amesema Ayoub na kuongeza…

“Tayari lipo tangazo la Serikali kuhusu mabadiliko ya nauli, lakini hatuwezi kulizungumzia hadi itakapoamuliwa vinginevyo, tutafanya usawa (balance), naamini huduma itarejea vizuri.”

Mmoja wa wananchi katika mtaa wa Sokoine, Said Hassan ameshauri kikao hicho kifanyike maeneo ya wazi ili kuwapa wananchi wa chini nafasi ya kushauri kutokana na maisha yao.

"Wasijifungie ndani kujadili ishu hii, waite mkutano wa wazi ili kila mwananchi aliye na nafasi aweze kushiriki na kutoa mapendekezo kwa mustakabali wa maisha yetu," amesema Hassan.

Chanzo: mwanachidigital