Baada ya kuzuka kwa sintofahamu baina ya taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela kukinzana na taarifa ya TRA kuhusu sababu za kuifungia bar ya The cask iliyopo mkoani humo jumuiya ya wafanyabiashara mkoani humo imefika katika ofisi za mkuu wa mkoa ili kujua ni lini itafunguliwa.
Baada ya kuzuka kwa sintofahamu baina ya taarifa ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilemela kukinzana na taarifa ya TRA kuhusu sababu za kuifungia bar ya The cask iliyopo mkoani humo jumuiya ya wafanyabiashara mkoani humo imefika katika ofisi za mkuu wa mkoa ili kujua ni lini itafunguliwa. Akizungumza baada ya kikao na Kaimu Katibu Tawala, Mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania mkoa wa Mwanza Patrick Masagati amesema kufikia kesho Agosti 22, 2023, wanatarajia kupata majibu iwapo itafunguliwa au la, ili nao watoe msimamo wao.