Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye mgogoro wa ardhi vijiji saba wamalizwa

11568 Hatimaye+pic TanzaniaWeb

Tue, 17 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ngorongoro. Hatimaye mgogoro wa ardhi baina ya vijiji saba vinavyounda Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) ya Makao na mwekezaji kampuni ya Mwiba Holdings Ltd, umepatiwa ufumbuzi.

Suluhusu hiyo imefikiwa baada ya kampuni ya Mwiba kuanza kulipa Sh610 milioni kwa mwaka kodi ya pango kwa vijiji na kuacha uvamizi wa kuingiza mifugo eneo la hifadhi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza katika ziara ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo eneo la Makao ya WMA, alisema baada ya mwafaka pande zote ziheshimu makubaliano.

Mtaka alisema Serikali kamwe haitakubali tena kuona watu wachache wanachochea migogoro katika eneo hilo.

“Tulifikia hatua mbaya hadi kutaka kumuondoa mwekezaji lakini binafsi nilikuwa najiuliza Simiyu utakuwa mkoa wa aina gani ambao hauna mwekezaji mkubwa?” alihoji.

Alisema walifikia hatua ya kumuomba Jaji Joseph Warioba na wengine kusuluisha lakini walikwama. “Sasa baada ya mwafaka na imebainika mambo mengi aliyodaiwa mwekezaji yalikuwa ni uongo kama ambavyo Serikali na viongozi wa CCM wabaini” alisema.

Awali, mmoja wa wakurugenzi wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund (FCF) ambayo kampuni zake ndizo zimewekeza katika wilaya hiyo ya Meatu, Abdulkadir Mohamed alisema kampuni za Mwiba Holding, Tanzania Game Trackers Safaris (TGTS) na Wingert Safaris wamewekeza zaidi ya Sh670 bilioni na mwaka huu wataongeza Sh227 bilioni.

“Tunatarajia kuongeza uwekezaji ila tunachoomba mazingira bora kwa kuondolewa migogoro katika maeneo yetu,” alisema.

ikiwepo uvamizi wa mifugo na kama kuna mapungufu tuelezwe,”alisema.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, Enock Yakobo alisema Chama Cha Mapinduzi kwa sasa hakina mgogoro na wawekezaji kwani mapungufu yaliyokuwepo yamekwisha na mafanikio yanaonekana.

Chanzo: mwananchi.co.tz