Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hatimaye Mzee Shirima azikwa Rombo

Rombo Pic Hatimaye Mzee Shirima azikwa Rombo

Fri, 16 Jun 2023 Chanzo: Mwananchi

Aliyekuwa Mwanzilishi na Mwenyekiti wa shirika la ndege la Precison Air, Michael Ngaleku Shirika (80) amezikwa Jana Juni 15 katika kijiji cha Nayeme wilayani Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.

Viongozi walioshiriki mazishi hayo ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa, Abdulrahman Kinana, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe, wafanyabiashara mashuhuri ndani na nje ya Mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wadau wengine.

Ngaleku alifariki gafla usiku wa Juni 9 katika hospitali ya Aghakan Dar es salaam alikokuwa amelezwa kwa ajili ya matibabu baada ya kulazwa Juni 8 mwaka huu.

Hata hivyo, mamia ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini wameshiriki katika mazishi hayo huku baadhi ya viongozi wakiitaka jamii kumuenzi Mzee Ngaleku kutokana na yale mazuri ambayo ameyaacha.

Profesa Mkenda amesema katika kumuenzi marehemu, kitabu chake alichoandika cha 'On my father's wings' kinachoelezea historia ya maisha yake kitatafsiriwa kwa lugha ya kiswahili na kusambazwa ili kila mmoja ajifunzae kupitia maisha yake.

"Taifa limepoteza mtu bingwa, aliyeacha historia nzuri katika Taifa hili," amesema Profesa Mkenda.

Kwa upande wake Makamu mwenyekiti wa CCM (Bara) Abdulraham Kinana amesema Mzee Ngaleku atakumbukwa sio kwa umaarufu wake bali kwa tabia njema.

"Binadamu tunapokuja duniani wote tuko sawa baadaye wengine wanapata vyeo, mali, madaraja na umaarufu lakin binadamu mzuri ni yule anayesemwa kwa tabia njema, kwa sifa nzuri za ubinadamu, si kwa cheo wala mali, sio kwa umaarufu bali shirima atakumbukwa kwa tabia njema,"

Mzee Ngaleku ameacha watoto wanne wakiwemo watatu wakiume na mmoja wakiume na wajukuu sita.

Chanzo: Mwananchi