Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hati za ardhi 283 zasajiliwa Ubungo

Silaa Ataka Mpango Uendelezaji Eneo La Viwanda Kibaha Hati za ardhi 283 zasajiliwa Ubungo

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

IKIWA ni siku tatu tangu kuzinduliwa kwa utoaji wa hatimilki za ardhi kupitia programu ya Ardhi Kliniki Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, hati 283 zimeshatolewa na migogoro ya ardhi 69 imetatuliwa.

Mratibu wa programu hiyo ya urasimishaji katika Manispaa ya Ubungo, John Ilomo ameeleza hayo alipokuwa akizungumzia muitikio wa wananchi kuchukua hati zao.

"Mpaka sasa tumefanikiwa kutoa hati hizi hii inaonesha kuwa wananchi wameelewa na wameitikia wito kufika kwenye viwanja hivi kwa ajili ya kujipatia hati, hakika wananchi wameelewa kuwa serikali imewasogeze huduma,” amesema.

Amesema japokuwa kuna hali ya mvua, lakini mwitiko wa wananchi umekuwa mzuri wanajitokeza hali inayoonesha kuwa walikuwa na uhitaji wa huduma hiyo karibu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live