Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hapi atoa siku 21 Tanroads, Tarura kumaliza barabara Airport ya Nduli

15710 Hapi+pic TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi ametoa siku 21 kwa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) pamoja na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS) kuhakikisha wanakamilisha ukarabati wa kipande cha barabara ya Uwanja wa Ndege wa Nduli, Iringa.

Kipande hicho kina urefu wa mita 250.

Ujenzi huo ni kwa ajili ya kuruhusu ndege kubwa za abiria kama vile Bombardier kutua bila matatizo na hivyo kuufanya mkoa wa Iringa kuwa kitovu cha utalii mikoa ya Nyanda za Juu Kusini.

Hapi ameyasema hayo leo Septemba 5 alipotembelea na kukagua maeneo mbalimbali ya uwanja huo wa ndege uliopo nje kidogo ya mji wa Iringa.

“Nawapa Tanroads wiki tatu kuhakikisha kipande hicho kinakamilika ili ndege kubwa zianze kutua na watalii na wawekezaji wakubwa waje kuwekeza,” amesema.

Kwa upande wake Meneja wa Uwanja  wa Ndege wa Nduli, Hanna Kibopile amesema tayari Sh480 milioni zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa barabara hiyo pamoja na maeneo mengine muhimu ikiwamo jengo la kusubiria abiria.

“Lengo kubwa la kufanya ukarabati kipande hicho korofi ni kuruhusu ndege kubwa kutua urefu wa barabara unatosha ndege kutua isipokuwa kile kipande korofi ndio kilikuwa kinaleta shida kuruhusu ndege kubwa kutua,”amesema.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz