Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hapi: Ole wake atakayenyanyasa wamachinga

15959 Hapi+pic TanzaniaWeb

Thu, 6 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Iringa. Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi amewacharukia polisi, mgambo na watendaji wengine wa Serikali akiwaonya kutothubutu kuwanyanyasa wamachinga.

Hapi (pichani) amesema yeyote atayewanyanyasa wamachinga hatabaki salama.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na wamachinga mkoani Iringa katika ukumbi wa Wel fear na kusema machinga ni mtu muhimu katika ukuaji uchumi nchini na kuwataka viongozi wa halmashauri kuwasaidia kufungua benki yao.

Alisema wamachinga ndio mtu pekee ambaye hana ubishi katika kuchangia maendeleo ya Serikali hivyo ameomba wasinyanyaswe wala kuingiliwa katika maeneo yao ya kazi kwa kupigwa na kunyang’anywa mali zao.

“Hayupo na hatakuwepo askari au mgambo wala mtumishi wa Serikali wa kuchaguliwa au kuteuliwa akawanyanyasa na kuwakandamiza machinga kwenye mkoa huu mimi nikiwa mkuu wa mkoa na akabaki salama.”

Hapi alisema Serikali ni ya wanyonge na viongozi wake wapo kuwatetea wananchi wanyonge, hivyo Jeshi la Polisi lisimame katika kulinda wananchi wanyonge na si kukandamiza wamachinga kwa sababu ndio watu pekee wanaoongoza katika kutoa kodi na kuchangia maendeleo hasa pato la taifa. Alisema imejengeka tabia kila mtumishi anataka afuatwe ofisini ndani ya uongozi wake anataka kila mtumishi aache kukaa ofisini akisikia malalamiko awafuate wamachinga si machinga wamfuate mtendaji.

“Sijaridhika na jinsi ambavyo mapato yanakusanywa viongozi wenu wamesema wamachinga hawana ubishi katika kuchangia maendeleo ya Serikali yao, taarifa za halmashauri zinaonyesha wamachinga 323 ndio wanachangia maendeleo na wanasema tangu mwezi wa saba mpaka mwezi huu wa 9 wamekusanya Sh9 milioni tu jambo ambalo haliridhishi kimahesabu,” alisema.

“Nawaagiza viongozi wa halmashauri kukaa na uongozi wa machinga na kutengeneza mfumo mzuri wa uchangiaji Serikali kuhakikisha fedha wanazotoa zinawafikia salama na iwe ni ndani ya mwezi mmoja mfumo huo uwe tayari umeanza kufanya kazi na fedha zitakazokusanywa zitumike kutengeneza taa za barabarani ili wamachinga wafanye biashara hadi saa nne usiku.”

Kwa upande wake katibu mtendaji wa umoja wa Machinga mkoa wa Iringa, Joseph Kilyenyi akisoma taarifa ya umoja wa machinga amesema wanauomba uongozi wa Jeshi la Polisi kuacha kuwanyanyasa machinga eneo la stendi ili kuwapa amani wafanyabiashara wa eneo hilo.

Alisema anawaomba halmashauri kuwapa nafasi ya kufanya magulio kama mikoa mingine wanavyofanya hata kwa siku chache na pia wakubaliwe kutengewa eneo la kufunga barabara hata siku moja ili wafanye biashara zao kama wengine.

Chanzo: mwananchi.co.tz