Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hapa ndipo atakapozikwa Said mume wa Swalha

Said Jeneza Mwili wa aliyejiua baada ya kumuua mkewe kwa risasi wachukuliwa mochwari

Wed, 1 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya ndugu na waombolezaji wamejitokeza kuchukua jeneza lenye mwili wa mkazi wa Buswelu, Said Oswayo aliyejiua kwa kujipiga risasi baada ya kumuua mkewe, Swalha Salum kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Oswayo anadaiwa kumuua mkewe kwa kumfyafulia risasi saba Mei 28,2022 kisha kutoweka nyumbani kwake huku mwili wake ukipatika Jumatatu Mei 30,2022 jioni ukielea ndani ya Ziwa Victoria katija ufukwe wa Rock Beach.

Picha ya Swalha Salum aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mmewe, Said Oswayo jijini Mwanza

Mwili huo umchukuliwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kilichopo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando na kusindikizwa na ndugu zake na wale wa upande wa mke wake.

Wakati mwili wa mkewe ukizikwa jana Mei 31, 2022 katika makaburi yaliyopo Kirumba mkoani hapa, mwili wa Said utapelekwa nyumbani kwake mtaa wa Mbogamboga kata ya Buswelu wilayani Ilemela mkoani Mwanza kabla ya kusafirishwa kwenda kijiji cha Etaro kilichopo wilaya ya Musoma mkoani Mwanza kwa ajili ya maziko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live