Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Handeni wazindua binti shujaa

60171 BINTI+PIC

Thu, 30 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Handeni. Ili kumaliza tatizo la mimba shuleni, wilaya ya Handeni imeanza kutekeleza kampeni ya ‘Binti Shujaa’ inayoenda sambamba na kuwachukulia hatua za kisheria wanaume wenye uhusiano wa kimapenzi na wanafunzi.

Mbali na kampeni hiyo, wameandaa utaratibu wa kila shule kuwa na washauri wa wanafunzi wanaoitwa bibi na babu ili iwe rahisi kwa watoto kujieleza na kusikilizwa wanapokuwa na changamoto.

Akizungumza katika maadhimisho ya wiki ya elimu wilayani hapa jana, mkuu wa wilaya hiyo, Godwin Gondwe alisema haiwezekani mimba ikawa chanzo cha kukatisha elimu ya msichana wakati upo uwezekano wa kuzuia.

Gondwe aliwataka wasichana kutokubali kudanganywa na chipsi ili wajiingize kwenye uhusiano wa kimapenzi bali wajikite kukamilisha ndoto zao. Alisema kiuhalisia hakuna mapenzi kati ya mwanaume na mwanafunzi na kwamba, iwapo wakibaini suala hilo linahesabika ni ubakaji.

Naye mkuu wa mkoa wa Tanga, Martine Shigella alisema mkoa huo umejipanga kuhakikisha unamaliza vikwazo kwa wasichana.

Shigella alisema mazingira mazuri ya kusomea ndiyo yatakayosaidia mkoa huo kufikia malengo yake kitaaluma.

Pia Soma

“Tunajenga madarasa ya kutosha ili watoto wapate elimu kwenye mazingira bora hii ndiyo njia mojawapo ya kuboresha elimu na kuhakikisha kila mwanafunzi anasoma,” alisema Shigela.

Awali, kaimu mwakilishi wa mtandao wa Elimu Tanzania (Tenmet), Clement Maganga alisema Handeni imechaguliwa kufanya maadhimisho hayo kutokana na mikakati yake ya kuboresha elimu hasa elimu jumuishi.

Maganga alisema tathmini yao inaonyesha wilaya za awali walizowahi kufanyia maadhimisho hayo ufaulu wake umeongezeka kwa sababu walichambua changamoto na kupata suluhisho.

Chanzo: mwananchi.co.tz