Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Handeni wavuna ziada mazao ya chakula

39c6641f8e2d2442767f5fe766622fdc Handeni wavuna ziada mazao ya chakula

Mon, 8 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Handeni, Toba Nguvila amesema wilaya hiyo haina njaa kutokana na kuwa na ziada ya chakula ambacho kimetokana na mavuno ya mahindi na mihogo katika msimu wa kilimo mwaka 2020.

Amesema kabla ya mavuno ya mahindi yaliyotokana na mvua za vuli zilizonyesha mwishoni mwa mwaka jana, wilaya hiyo ilikuwa na ziada ya tani takribani milioni moja za mihogo.

Nguvila alisema hayo wakati alizungumza na HabariLEO mwishoni mwa wiki lililotaka kujua wilaya hiyo ina mikakati gani wa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli alilolitoa hivi karibuni kwa wakuu wa wilaya zote nchini kuhakikisha kila wilaya inajitosheleza kwa chakula kwani hakutakuwa na chakula cha msaada.

"Nataka nikufahamishe kuwa kwa sasa hivi wilaya ya Handeni hakuna njaa, tumejitosheleza kwa chakula, tuna mahindi ya vuli ambayo wananchi wanavuna na mihogo ya kutosha."

"Kuhusu mihogo wakulima wamelima kwa wingi zaidi ya hekta 500, tunawashukuru benki ya NMB ambao waliwakopesha wakulima wa mihogo Sh bilioni 3.2 mwaka jana kwa ajili ya kundeleza kilimohicho na sasa hivi tuna ziada ya tani milioni moja," alisema.

Mkuu huyo wa wialaya alisema kutokana na mihogo kuwa mingi, zao hilo limeshuka bei wilayani humo, ambapo kwa sasa gari la tani 2.5 likijaa ni Sh 800,000 kutoka Sh 250,000.

"Kutokana na ziada hiyo tunaweza kusema sisi Handeni tumelitekeleza agizo hilo ingawaje bado tutawahamasisha wananchi waandae mashamba kwa ajili ya kilimo cha msimu wa mvua za masika," alisema.

Kuhusu kilimo cha mkonge, alisema kuwa katika kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kuzitaka halmashauri zinazolima zao hilo kutenga maeneo kwa ajili kupanda mkonge, benki za NMB, CRDB na TIB zimekubali kuwakopesha wakulima wa zao hilo ili kuendeleza kilimo hicho.

Chanzo: habarileo.co.tz