Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri zatakiwa kutenga 10% kuhifadhi mazingira

A7e2aeb401f9b0a161b35d74edbd24d5 Halmashauri zatakiwa kutenga 10% kuhifadhi mazingira

Thu, 18 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

HALMASHAURI zote nchi zimetakiwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya shughuli za uhifadhi na usimamizi mazingira katika maeneo yao.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira),Mwita Waitara, alitoa agizo hilo kwa nyakati tofauti alipofanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mji na Wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Waitara alisema kutengwa kwa fedha hizo kutazisaidia halmashauri kupata vitendea kazi vitakavyotumika katika usafi wa mazingira.

“Huwezi kusema unazoa taka wakati huna hata vitendea kazi, kwa hiyo halmashauri zinapaswa kutenga asilimia kumi ya bajeti za kutokana na mapato ya ndani kwa mwaka na kuweka mikakati ya kutunza mazingira,” alisema Waitara.

Alizitaka halmashauri zote kuunda vikundi vitakavyojihusisha na uzoaji wa taka mitaani ili kuweka mazingira katika hali ya usafi.

Pamoja na maagizo hayo, Waitara aliipongeza Halmashauri ya Nzega kwa kulipa kipaumbele suala la mazingira.

Kwa sasa kupitia mapato ya ndani, hiyo imetenga fedha kwa ajili ya kununua gari la kukusanya na kusafirisha taka.

Aliipongeza Nzega kwa kutekeleza agizo la Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan la kuzitaka halmashauri kupanda miti milioni moja kila moja.

Chanzo: habarileo.co.tz