Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri ya Wilaya ya Busega imeteketeza vifaa haramu vya uvuvi

NYAVU.webp Halmashauri ya Wilaya ya Busega imeteketeza vifaa haramu vya uvuvi

Wed, 10 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

OFISI ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, imekamata na kuteketeza nyavu 110 na kokoro 2 zilizokuwa zinatumika katika uvuvi haramu katika vijiji vya Nyakaboja na Maega mkoani humo.

Kutokana na kukithiri kwa uvuvi haramu katika ukanda wa Ziwa Victoria, Ofisi hiyo imeanza zoezi la kupambana na wavuvi hao wanaotumia vifaa visivyokubalika katika shughuli za uvuvi ili kuzuia uharibifu wa rasilimali katika ziwa hilo.

Aidha, Ofisi hiyo ya Mkurugenzi Mtendaji imewataka wavuvi wote wilayani humo kufuata sheria za uvuvi kwa kufanya shughuli zao za uvuvi kwa kufuata utaratibu uliowekwa na serikali, kwani uvuvi haramu unachangia kushuka kwa ukusanyaji wa mapato nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live