Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri ya Songea yapewa siku 14 kuhakiki madeni ya watumishi

Ndejembi Ed Halmashauri ya Songea yapewa siku 14 kuhakiki madeni ya watumishi

Sun, 10 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Deogratias Ndejembi, ametoa siku 14 kwa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuhakisha kuwa anafanya uhakiki wa madeni yote ya watumishi na kuyawasilisha katika Ofisi ya Rais Utumishi ili waweze kulipwa haki zao.

Ndejembi ametoa agizo hilo alipofanya ziara katika Manispaa hiyo kwa ajili ya kuzungumza na watumishi wa umma lengo likiwa kusikiliza changamoto zao na kuzitatua kwa muda huo.

Akijibu changamoto ya malimbikizo ya mishahara ambayo wanadai watumishi hao, Naibu Waziri Ndejembi amesema Wizara ya Utumishi imekua ikilipa madeni hayo kwa haraka pindi ambapo wamekua wakiletewa orodha ya watumishi wanaodai na kwamba watumishi wanapoona wamechelewa kulipwa wajue shida haipo wizarani bali ipo kwa Maafisa Utumishi kwani wao ndio wamekua wakichelewesha upelekaji wa majina.

“Natoa siku 14 mpaka ifikapo Oktoba 22, 2021 Afisa Utumishi wa Manispaa ya Songea na wengine wote nchini sisi Ofisi ya Rais Utumishi tuwe tumepata madeni ya watumishi wote wa Manispaa ya Songea wanaostahili kulipwa ili tuweze kuyafanyia uhakiki yaweze kurudishwa, Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inajali watumishi wake hivyo tuleteeni majina tuyahakiki na kuyapeleka hazina ili waweze kulipwa wote haki yao”

Maafisa Utumishi harakisheni kufanya uhakiki na kutuletea orodha hizo, hizi ni haki za watumishi wetu siyo hisani ni jasho lao hivyo wanapaswa kulipwa stahiki zao, na nitoe wito pia Kwa Watumishi wote wenye kudai fuatilieni majina yenu kwa Maafisa Utumishi ili ndani ya hizo wiki mbili nilizotoa tuweze kupata orodha yenu na kuifanyia kazi” amesema Naibu Waziri Ndejembi.

Chanzo: ippmedia.com