Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri ya Mji Kondoa yatekeleza agizo la Jafo

028995b9076e72081367331e58af5ef6 Halmashauri ya Mji Kondoa yatekeleza agizo la Jafo

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Mji wa Kondoa mkoani Dodoma, imetekeleza agizo la Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tsamisemi), Selemani Jafo la kuhamia katika jengo lao jipya la utawala lililogharimu Sh bilioni tatu.

Akizungumza baada ya kuhamia kwenye jengo hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kondoa Mji, Msoleni Dakawa alisema jengo hilo litarahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Alisema kwa sasa watafanya kazi kwa kasi na kwa karibu, kwa kuwa idara zote zitakuwa zipo pamoja.

Dakawa alisema kwa sasa watakuwa pamoja, tofauti na jengo la zamani ambako walikuwa wamepanga na idara zilikuwa zimetawanyika, hivyo kusababisha washindwe kutoa huduma kwa wakati kwa wananchi.

Mkurugenzi huyo alisema kuhamia katika jengo hilo la utawala ambalo ni la kisasa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Jafo alilotoa Desemba 2020 ambapo aliagiza halmashauri hiyo kuhakikisha watumishi wake wanahamia ifikapo mwaka 2021. Alitoa agizo hilo baada ya kukagua na kujiridhisha kuwa jengo hilo limekamilika.

Alisema hapo awali halmashauri hiyo ilikuwa imepanga kwenye jengo la serikali ambalo ni la zamani. Jengo hilo lilikuwa halikutoshelezi kuhudumia wananchi na pia lilikuwa halitoshelezi mahitaji ya watumishi wenyewe.

“Sasa tumepata jengo letu wenyewe la Halmashauri ya Mji wa Kondoa, hivyo watumishi wenzangu tulitumie jengo hili kuwahudumia wananchi kwa uwazi na sio vinginevyo, mzingatie kuwa fedha zilizojenga jengo hili zimetoka serikalini,”alisema.

Kwa upande wao, wananchi wa wilaya ya Kondoa waliipongeza serikali kwa kuwezesha halmashauri hiyo kuwa na jengo la kisasa badala ya jengo la zamani ambalo lilikuwa halitoshelezi.

Mmoja wa wananchi hao, Ayubu Lubuva alisema wanaipongeza Serikali ya Rais John Magufuli ambaye amewezesha ujenzi wa jengo hilo la halmashauri, ambalo litahudumia Watanzania kwa weledi.

Chanzo: habarileo.co.tz