Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Halmashauri tengeni fedha kwa lishe ya watoto’ RC Shinyanga

1dd7dc61baef838b995426832841dadb.jpeg ‘Halmashauri tengeni fedha kwa lishe ya watoto’ RC Shinyanga

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga, Dk Philemon Sengati, amezitaka halmashauri zote za mkoa huo kutenga fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya lishe kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano.

Alisema hayo jana katika kikao cha kujadili tathmini ya hali ya lishe huku akisema zinahitajika dhamira za dhati kufikia hatua nzuri katika utekelezaji wa shughuli za lishe.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) mwaka 2018, udumavu katika Mkoa wa Shinyanga kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano umeongezeka kutoka asilimia 3O hadi asilimia 32.1.

Sengati alisema takwimu za ukondefu kwa watoto pia zimeongezeka kutoka asilimia mbili hadi 4.3 na kuongezeka kwa uzito kwa watoto hao kumepungua kutoka asilimia 22 hadi 15.

Aliwataka viongozi wa halmashauri kutenga Sh 1,000 kwa kila mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano.

"Halmashauri ya Kishapu ndio inaonekana kufanya vibaya kwenye afua za lishe," alisema.

Akizungumzia suala la wilaya yake kutofanya vizuri katika eneo la lishe, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Joseph Mkude, alisema si vigezo vyote ambavyo wilaya yake imeshindwa kufanya vizuri, bali upungufu umejitokeza katika eneo la uchangiaji Sh 1,000 kwa kila mtoto chini ya miaka mitano.

Mkude alisema moja ya hatua muhimu atakazofanya wilayani kwake ni kumhimiza mkurugenzi kuweka dhamira ya dhati katika suala hilo sambamba na kutoa elimu zaidi kuhusu masuala ya lishe kwa jamii.

Chanzo: www.habarileo.co.tz