Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri nne matatani kwa kukiuka sheria ya manunuzi

Kampunipic Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba

Wed, 29 Sep 2021 Chanzo: Mwananchi

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuzifanyia ukaguzi na uchunguzi wa kina halmashauri nne na taasisi moja kwa kukiuka sheria za ununuzi wa umma.

Amezitaja halmashauri hizo kuwa ni ya Mji Kondoa mkoani (Dodoma), Biharamulo (Kagera), Mbogwe na Chato (Geita) na Taasisi ya Utafiti wa Wanyama.

Dk Mwigulu ametoa maagizo hayo leo Jumatano Septemba 29, 2021 baada ya kupokea ripoti ya tathimni ya utendaji ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ya mwaka wa fedha 2020/2021.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano Serikali cha Wizara ya Fedha na Mipango Dk Mwigulu ameagiza kuchukuliwa kwa hatua za kisheria kwa watu wote ikiwemo

waliotoa nje ya Mfumo wa Ununuzi wa Umma kwa njia ya Mtandao (TANePS) unaotumika kuchakata zabuni.

Aidha, Dk Mwigulu amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba, kuziandikia waraka taasisi 172 ambazo zimeunganishwa kwenye mfumo TANePS lakini hawautumii ili watoe sababu za kutotumia mfumo huo katika kufanya ununuzi.

Alizitaka pia taasisi za ununuzi zote kutumia asilimia 30 ya gharama yote ya zabuni zinazotangazwa katika mpango wao wa ununuzi wa mwaka kwa ajili ya kuyawezesha makundi maalumu yakiwemo ya vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu kwa mujibu wa sheria ya ununuzi.

“Nimesikitika sana baada ya kusikia kwamba kati ya taasisi 86 mlizozikagua ni Taasisi mbili tu ndizo zilitenga asilimia 30 katika mpango wao wa ununuzi wa mwaka kwa ajili ya makundi maalumu,” amesema.

Mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa PPRA kwa niaba ya Mwenyekiti wa bodi hiyo, Profesa Ninatubu Lema amesema taasisi tano zilipata wastani hafifu wa kufuata sheria taratibu na kanuni za ununuzi wa umma.

Lema amesema katika mwaka wa fedha 2020/2021 walifanya ukaguzi wa mikataba 8,838 ya ununuzi yenye thamani ya Sh9.2 trilioni kutoka taasisi 86.

Kwa upande wake Tutuba katika mwaka 2020/2021, bajeti ya ununuzi ilikuwa Sh25 trilioni sawa na zaidi ya asilimia 75 ya bajeti yote ya Serikali.

Chanzo: Mwananchi