Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri Temeke kuwasomesha wanafunzi wawili waliong’ara kidato cha sita

67066 HALMASHAURI+PIC

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imeahidi kuwasomesha wanafunzi wawili waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita mwaka 2019.

Imesema lengo ni kuwahamasisha wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihani yao.

Wanafunzi hao ni wa Shule ya Sekondari Temeke, Satrumin Shirima aliyeshika nafasi ya sita kitaifa katika masomo ya Sayansi na  Salma Shekimweri aliyeshika nafasi ya tisa katika orodha ya wanafunzi 10 waliofanya vyema masomo ya biashara.

Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa hiyo, Ludubilo Mwakibibi amesema wanafunzi hao watasomeshwa na halmashauri hiyo, watalipiwa kila kitu na kuondokana na mkopo wa elimu ya juu.

Katika matokeo hayo Shirima amepata alama A katika masomo ya Biolojia, Kemia na Fizikia huku  Salma akipata A somo la Biashara na B katika somo la Uchumi na Biashara.

Mwakibibi amesema wataitisha kwa dharura kamati ya fedha ili kujadili kutenga fedha kwa ajili ya gharama za masomo ya wanafunzi hao.

Pia Soma

"Naagiza watoto hawa wafunguliwe akaunti ya benki ili kila mmoja aweze kuingiziwa fedha,” amesisitiza.

Shirima ameishukuru halmashauri hiyo kwa kuwapa ufadhili kwa maelezo kuwa utaipunguzia familia yake majukumu huku Salma akiahidi kusoma kwa bidii ili atakapomaliza chuo arejee  katika halmashauri hiyo kufanya kazi kwa lengo la kurudisha fadhila.

Chanzo: mwananchi.co.tz