Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri Moshi yafungasha virago yahamia Kolila

Tue, 15 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Halmashauri ya Moshi imetangaza kuhamishia ofisi zake eneo la Kolila umbali wa kilomita sita kutoka zilipo sasa.

Eneo la Kolila ndiko yalipokuwa makao makuu ya mkoa wa Kilimanjaro enzi za wakoloni wa Kijerumani, yalihamia Moshi baada ya ujio wa reli ambayo haikuweza kupanda eneo la mwinuko.

Uamuzi huo wa halmashauri hiyo kuhamishia ofisi zake zote zilizopo KDC manispaa ya Moshi, ulifikiwa mwishoni mwa wiki iliyopita katika kikao cha dharura cha Baraza la Madiwani.

Hatua hiyo ni kutekeleza agizo la Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo alilolitoa kwa halmashauri 31 kuhamishia ofisi zake maeneo ya utawala ndani ya siku 30.

Jafo alitoa agizo hilo baada ya Rais John Magufuli akiwa mkoani Rukwa, kuagiza halmashauri ya Sumbawanga Vijijini kuhamia Laela na halmashauri zingine zote kuhamia maeneo yao ya utawala.

Katika agizo lake, Rais Magufuli aliagiza mkurugenzi au mtumishi atakayegoma kuhama afukuzwe mara moja, huku Jafo akienda mbali zaidi kuwa halmashauri itakayogoma itafutwa.

Pia Soma

Advertisement
Mwenyekiti wa halmashauri ya Moshi inayohudumia majimbo ya Vunjo na Moshi Vijijini, Michael Kilawila alisema wameamua kuhamishia ofisi zao kutekeleza agizo la Serikali.

Naye mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Castori Msigala alisema kamati ndogo iliyoundwa ilipendekeza eneo hilo kwa sababu ya gharama ndogo za kuhamia.

Chanzo: mwananchi.co.tz