Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Halmashauri Madaba yatoa mikopo zaidi ya milioni 53/-

B71e76e06f4770df1bb5adc1f064c050 Halmashauri Madaba yatoa mikopo zaidi ya milioni 53/-

Thu, 21 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

HALMASHAURI ya Wilaya ya Madaba imetoa mkopo wa Sh 53,278,000 sawa na asilimia 85 kutoka mapato ya ndani kwa vikundi 15 katika awamu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2020/21.

Kati ya vikundi hivyo, 13 ni vya wanawake na viwili ni vya vijana.

Kaimu Ofisa Maendeleo ya Jamii wa halmashauri hiyo, Bashiru Mgwassa juzi alisema vikundi hivyo ni vile vinavyojishughulisha na kilimo, usindikaji na biashara, ambapo jumla ya wanufaika wa mikopo hiyo ni watu 205, vijana wakiwa 45 na wanawake 160.

Alisema mkopo huo ni awamu ya kwanza kwa mwaka wa fedha 2020/21 na malengo ya halmashauri ni ifikapo Juni mwaka huu itatoa tena mkopo wa awamu ya pili ili kufikiwa lengo la asilimia 100 kulingana na bajeti ya mwaka 2020/21 kupitia mapato ya ndani ambapo wamekadiria kutoa Sh milioni 74.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Madaba, Shafi Mpenda alisema kutokana na changamoto kadhaa wamelazimika kutoa Sh milioni 53 ambazo ni pungufu ya Sh milioni 20.72, lakini mpango wa halmashauri kabla ya kufungwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, 2021 fedha hizo zitatolewa kwa vikundi vilivyobaki.

Chanzo: habarileo.co.tz