Halmashauri tatu zinazonufaika na hifadhi ya Waga zimetakiwa kutenga bajeti kupitia mapato yao ya ndani kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili hifadhi hiyo.
Halmashauri hizo ni pamoja na Mbarali ya Mkoa wa Mbeya, Iringa Vijijini na Mufindi mkoani Iringa.
Wito huo umetolewa jana Jumanne 27, 2023 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali, Missana Kwangura wakati wa mjadala mpango wa miaka 10 wa usimamizi ya hifadhi ya wanyapori (GMP) katika warsha ya wadau wa Jumuiya ya Wanyapori ya Waga iliyofanyika wilayani Mufindi.
Amesema kila halmashauri inauwezo wa kutenga bajeti na kuzipeleka katika idara za Maliasili, Kilimo na Mifugo kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo uwekaji wa mipaka kati ya wananchi na hifadhi hiyo.
"Sisi kama halmashauri tunaweza kutenga bajeti kupitia mapato yetu ya ndani ili kutatua changamotoyauwekaji wa alama za mipaka hekta 31 kwa kuanza kwa awamu ili baada ya muda fulani tukamilishe," amesema Kwanguru.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Kenny Shilumba amesema kuwa mpango huo unaweza kusaidia kufanya Mikutano kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi kuhusu utunzaji wa hifadhi hiyo.
"Elimu zaidi inahitajika kwa wananchi kwa sababu wakiwa na Elimu ya kutosha watakuwa wahoga hivyo itasaidia kutunza hifadhi zetu bila ya wao kujuwa," amesema.
Naye Kamishna Mhifadhi Msaidizi wa Mammalaka ya Usimamizi wa Wananyapori Tanzania (Tawa), Martha Msemo amesema kuwa watahakikisha wanashirikiana kwa pamoja na halmashauri hizo ili wananchi waweze kupata elimu hiyo kwa upana zaidi.
"Kazi hii ya utoaji wa elimu kwa wananchi hatuwezi kufanya pekee yetu hivyo ni lazima tushirikiana kwa pamoja na halmashauri zote zilizopo katika hifadhi ya Waga kwa sababu sisi tuna kitengo cha Uhamasishaji kwa jamii kwa ajili ya kutoa elimu," amesema Msemo.