Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali si Shwari Dodoma

Dodomapic Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka

Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Anthony Mtaka amewataka wakazi wa Dodoma kuchukua hatua za tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona kwa sababu hali si nzuri mkoani humo.

Ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 3, 2021 wakati akizungumza na askari wa usalama wa barabarani na viongozi wa masoko wa mkoa wa Dodoma, huku akiwataka wahakikishe wanachukua hatua za kujikinga na ugonjwa huo kwa kuvaa barakoa na kunawa mikono kwa maji yanayotiririka kwa kutumia vitakasa mikono.

Pia amewataka askari wa usalama wa barabarani kuhakikisha watu wote wanakaa kwenye viti (level seat) kwenye daladala na bajaji na kwenye bodaboda kuhakikisha hawabebi abiria zaidi ya mmoja.

Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Dodoma, Boniface Mbao amesema watakapotoka katika kikao hicho wataenda kutekeleza maagizo hayo kwa kutoa elimu na ikibidi kwa ukali, ili kuhakikisha abiria wanakaa katika viti kwenye mabasi ya abiria.

Amesema hakuna gari litakalopita kwenye mkoa huu likiwa limejaza zaidi ya abiria waliokaa kwenye viti

Chanzo: www.tanzaniaweb.live