Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hali ilivyo nyumbani kwa Mzee Mrema

Mremaaaaa Hali ilivyo nyumbani kwa Mzee Mrema

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka Mtaa Kilimahewa, Salasala jijini Dar es salaam, hapa nyumbani kwa mwanasiasa nguli wa mageuzi na Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Mzee Augustino Lyatonga Mrema ambaye alifariki dunia jana Agosti 22, akiwa na umri wa miaka 77.

Mrema amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha TLP, Augustino Mrema anatarajiwa kuzikwa Alhamisi Agosti 25, katika kijiji cha Kiraracha mkoani Kilimanjaro

Maziko hayo yatatanguliwa na ibada ya mazishi siku ya Jumatano itakayofanyika katika Kanisa Katoliki Parokia ya Salasala kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro.

Hayo yameelezwa leo Jumatatu Agosti 22, 2022 na mwanaye, Michael Mrema wakati akitoa ratiba ya msiba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live