Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Hakuna mgawo wa maji Iringa- IRUWASA

Maji Mgao (600 X 365) Hakuna mgawo wa maji Iringa

Sun, 21 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Iringa (Iruwasa) imewahakikishia wateja wake kuwa wataendelea kupata huduma ya maji na hakutakuwa na mgawo kama ilivyo katika maeneo ya mikoa mininge.

Imesema kuwa tangu kukamilika kwa mradi wa maji mwaka 2012 uliogharimu zaidi ya Sh70 bilioni, asilimia 97 ya wakazi wa Manispaa ya Iringa wanapata huduma ya maji safi.

Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano cha Iruwasa, Restituta Sakila amesema hakutakuwa na mgawo wa maji katika Manispaa hiyo.

“Tulikuwa tunahofia mgawo wa umeme kwamba unaweza kusababisha maji kuwa na mgawo, lakini kama umeme ni wa uhakika hakutakuwa na mgawo wa maji. Yaliyopo yanatosha kwa asilimia 97,” amesema Sakila.

Amewataka wakazi wa Mkoa huo kutunza mazingira kwa kuwa shughuli za kijamii zinaathiri vyanzo vya maji hasa kwenye mto Ruaha Mdogo.

“Kule wanafyatua tofari, wanalima hii ni hatari. Maji ya Mto Ruaha Mdogo yanahudumia watu wengi zaidi na ikiwa hawatatunza siku za usoni, hali inaweza kuwa mbaya,” amesema

Ofisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Mkoa wa Iringa, Francis Mbelwa amesema maeneo ya huduma za jamii kama hospitali na yalikotegeshewa mitambo ya maji hakutaathiriwa na mgawo wa umeme.

“Hatuwezi kukata umeme sehemu inayotoa huduma za kijamii, kwa hiyo tunayajua maeneo ambayo Iruwasa imeweka mitambo yake ya maji,” amesema.

Chanzo: mwananchidigital