TAARIFA RASMI YA MKUU WA WILAYA
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Dkt. Vincent Anney amesema “Ni tukio la kweli, Hakimu alikuwa na mgogoro na Wanakijiji, yeye si mwananchi wa Rungwe ila alinunua eneo Rungwe.
“Zamani baba yake alikuwa anaishi Rungwe akahamia Kyela, hata yeye Hakimu alizaliwa hukohuko Kyela. Hapo kati alianzisha mgogoro na wananchi akisema anataka eneo la babu yake lakini hiyo ni sehemu nyingine, si seheu amayo tukio limetokea.
“Eneo ambalo limesababisha auawe ni kubwa kuna karibia ekari 1000, ni msitu na ni hifadhi ambayo imekuwa ikisadia mvua, alinunua kinyemela, wananchi wakamshtaki Mahakamani.
“Akashindwa kesi, alikuwa katika harakati za kukata rufaa, kesi ikiwa imeisha akaenda shambani akiwa na watu wengine wawili akaanza kuchimbachimba, inasemakana alikuwa anachimba dawa.
“Yakatokea majibizano kati yake na Wananchi waliofika eneo hilo, akatoa bastola na kuwapiga risasi Wananchi wawili miguuni.
“Wananchi wakakasirika na kuanza kumpiga kisha kusababisha kifo chake pamoja na mmoja kati ya wale watu wawili alioongozana nao, mwingine mmoja alitokomea haijulikani alipokwenda.
“Tumeshawakamata watu kama saba hivi kutokana na tukio hilo na uchunguzi unaendelea.”