Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

HUDUMA MAJI SAFI MKURANGA HADI APRILI 2021.

302cdaa61e9cbf74ee54cfe5a50ee9a1 HUDUMA MAJI SAFI MKURANGA HADI APRILI 2021.

Wed, 2 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Wananchi wa Wilaya ya Mkuranga na maeneo jirani wapo mbioni kuondokana na adha ya ukosefu wa maji ya uhakika kutokana na ujenzi wa mradi wa maji ulioigharimu Serikali kiasi cha zaidi ya Sh Bilioni 2 wilayani humo, kufikia zaidi ya asilimia 90 ya utekelezwaji wake.

Hayo yamebainishwa na Meneja usimamizi wa mradi huo,Mhandisi Erasto Mwakilulele alipokuwa akitoa taarifa ya ujenzi wa mradi huo kwa Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa wilayani humo.

Alisema matarajio ya wananchi wa wilaya hiyo kuanza kupata maji kutoka katika mradi huo, ni kuanzia Februari Mwakani mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa eneo litakalofungwa pampu za kusukuma maji ambapo ujenzi wake umefikia asilimia 30 hadi sasa.

Chanzo: habarileo.co.tz