Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gongwe: Msinyanyase wanawake kisa 'Chagulaga'

Gondwe Pic Gongwe: Msinyanyase wanawake kisa 'Chagulaga'

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, Godwin Gondwe amekemea vikali tabia ya Vijana wa kiume kudhalilisha kingono Wasichana Wilayani humo kwa kuwalazimisha kufanya nao mapenzi na kuwaoa bila ridhaa yao kwa kisingizio cha utamaduni wa kisukuma wa Chagulaga.

Akiwa kwenye mkutano wake na Wananchi, DC Gondwe amewapa nafasi Wananchi kutoa maoni kuhusu tamaduni hiyo ambapo Mwanamke mmoja amesema “Niliona umeisha mnada jioni, Vijana wakawa wanawakimbiza Wadada, wakawazingira Wadada wawili wakawasumbua mpaka mashati yamechanika”

Baada ya kusikiliza michango ya Wananchi kadhaa, DC Gondwe akanukuliwa akisema “Haiwezekani Wanaume kumi au ishirini wanawakimbiza Wanawake wawili wanasingizia mwavuli wa utamaduni wa Chagulaga haiko hivyo, tutawatafuta hao Vijana wanaosingizia utamaduni kunyanyasa Mabinti”

Utamaduni huo uliopitwa na wakati umeripotiwa mara kadhaa katika baadhi ya Wilaya za Morogoro (Ulanga) na Bahi Mkoani Dodoma na kupigwa marufuku na Viongozi, ambapo Vijana wa Jamii ya wafugaji wa kabila la Wasukuma huwalazimisha Wanawake kufanya nao mapenzi na kuwaoa bila ridhaa yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live