Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gondwe awataka wafanyabiashara kutoa risiti

6ea397a40b77e95f61e999fe39c531af Gondwe awataka wafanyabiashara kutoa risiti

Fri, 12 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amewataka wafanyabiashara kutoa risiti pindi wanapouza bidhaa au kutoa huduma yoyote kwa wateja wao.

Gondwe amebainisha hayo leo mkoani Dar es Salaam alipokuwa sambamba na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) waliokuwa wanaanza kampeni ya elimu ya mlipa kodi wilayani humo.

“Nawahasa wafanyabiashara kutunza kumbukumbu za biashara zao na kutoa risiti kwa wateja pindi wanapouza bidhaa au kutoa huduma yoyote kwani itawasaidia kujua kiasi cha kodi wanachotakiwa kulipa” amesema Gondwe.

Katika hatua nyingine Gondwe ameipongeza TRA kwa kuendesha kamapeni ya elimu kwa mlipa kodi wilayani humo kwani itawasidia wafanyabiashara kuwa na uelewa katika masuala ya ulipaji kodi.

Chanzo: www.habarileo.co.tz