Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gondwe atoa wiki moja Barabara ya Keko kuboreshwa

12cc2386ba4aceb1beb4201e972a1b4d Gondwe atoa wiki moja Barabara ya Keko kuboreshwa

Sat, 6 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe ametoa wiki moja kwa Mkandarasi kuhakikisha anaifanyia marekebisho Barabara ya Keko ili iweze kupitika kiurahisi.

Gondwe ametoa gizo hilo leo alipofanya ziara kukagua barabara hiyo wilayani humo mkoani Dar es Salaam na kubainisha kuwa barabara hiyo imekuwa kero kubwa kwa wakazi wa Temeke.

"Hii ni Barabara ambayo ipo kwenye mpango wa kupita magari yaendayo kasi, moja ya makubaliano katika mkataba ni kufanya marekebisho madogomadogo na tayari TANROADS wamewakabidhi, hatuwezi kukaa kusubiri, nimewapa siku saba Wakandarsi watengeneze ili Wananchi wa Temeke waendelee na kazi zao"amesema Gondwe

Chanzo: www.habarileo.co.tz