Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gondwe: Sitakubali Magufuli ahujumiwe

2713412fed8b8e9c0edf9a7416d1c77b Gondwe: Sitakubali Magufuli ahujumiwe

Thu, 11 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe, amesema hatakubali mkandarasi anayejenga barabara ya mabasi yaendayo haraka kuanzia Gerezani hadi Mbagala amhujumu Rais John Magufuli.

Gondwe jana alikasirishwa na kitendo cha mkandarasi huyo, kampuni ya Sino Hydro kutoka China kuijenga barabara hiyo chini ya kiwango na kwa kusuasua.

Alitoa msimamo huo alipokagua ujenzi wa barabara hiyo na kueleza kuwa, mkandarasi huyo ameonesha mapungufu makubwa katika utendaji wake kwa kuwa barabara hiyo ina nyufa nyingi wakati haijakamilika na haijaanza kutumika.

“Naagiza msimamizi wa mradi huu ambaye ni Wakala wa Barabara Tanzania TANROADS kuhakikisha mapungufu yote yaliyojitokeza yanarekebishwa mara moja ikishindikana taratibu za kisheria zifuatwe ili aondolewe.” alisema Gondwe.

Katika ziara hiyo iliyoanzia aneo la makutano ya reli na bandari jijini Dar es Salaam Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Temeke ikiongozwa na Gondwe ilitembelea na kukagua ujenzi wa barabara hiyo na vituo vya mabasi hayo.

Alisema jkatika ziara hiyo kuwa mkandarasi huyo amekua na kiburi na anaendelea kuihujumu nchi kwa sababu anadiriki kubadili matokeo ya uchunguzi wa kimaabara unaoonesha kuwa kazi zake ziko chini ya kiwango, na anafukuza watanzania wanaotoa taarifa za kuhujumiwa kwa mradi.

“Nimepata taarifa kuwa sampuli za udongo zilizochukuliwa na wataalamu hapa katika eneo la Mgulani zilikataa na walitakiwa warudie ujenzi wa tabaka la chini la hii barabara lakini wao walikwenda kubadilisha matokeo na wakawatishia wataalamu wetu na wengine wakawafukuza kazi hii si sawa hata kidogo katika utawala huu wa JPM” alisema Gondwe.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka, Ronald Lwakatare, alisema barabara hiyo ni muhimu kwa maisha ya wakazi wa Mbagala na maeneo ya jirani hivyo ni lazima ijengwe kwa kiwango cha kimataifa ili idumu kwa miaka mingi.

Alisema zaidi ya Shilingi bilioni 217 zinatumika katika mradi huo hivyo ni vyema kasi ya utekelezaji iongezeke ili wakazi wa Mbagala waanze kufurahia usafiri wa mabasi yaendayo haraka.

Chanzo: habarileo.co.tz