Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gondwe: Daraja halitavinja ndoa zenu tena

Gondwe Pic Gondwe: Daraja halitavinja ndoa zenu tena

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, Godwin Gondwe amesema ujenzi wa daraja linalounganisha Vijiji vya Nkulagano na Chimendeli utasaidia kukuza shughuli za kiuchumi lakini pia kuokoa ndoa za Watu kwakuwa baadhi ya Wanaume walikuwa wanachepuka kwenye ndoa zao kwa kisingizio cha uwepo wa daraja la zamani ambalo halikuwa bora.

“Mvua ikinyesha wa Chimendeli wanakwenda zao Nkulagano na wa huku wanaenda kule, mvua ikinyesha anasema ‘Oh Mama siji tena daraja limeziba’ akina Mama walikuwa wanalalamika Wazee wakiwnda Kijiji kingine, sababu zilikuwa daraja, Mama Samia kaleta suluhisho kesi hizo sitaki kuzisikua tena, kero kubwa ilikuwa daraja”

DC Gondwe amesema kuwa Serikali imetoa fedha za ujenzi wa daraja jipya ambalo limejengwa kwa mawe lenye thamani ya Tsh. milioni 400 “Kama lingejengwa kwa zege lingegharimu Tsh. bilioni 3., hivyo Serikali hapa imeokoa takribani bilioni 2 na milioni 600”

“Mkandarasi yupo asilimia 51, angetakiwa kuwa asilimia 20 ila amekwenda kasi zaidi, tunampongeza Makandarasi ni JP Traders”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live