Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ghorofa laporomoka na kuua mmoja Kigamboni

Ghorofazz (4).jpeg Ghorofa laporomoka na kuua mmoja Kigamboni

Wed, 17 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaume mmoja ambaye ni Fundi wa ujenzi aliyefahamika kwa jina moja la Omary maarufu Mwarabu amefariki dunia na Mafundi wenzake wanane wamejeruhiwa baada ya jengo la ghorofa mbili ambalo walikuwa wanaendelea kulijenga kuporomoka leo April 17, 2024 katika Mtaa wa Magogoni Wilayani Kigamboni Mkoa wa Dar es salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amefika eneo la tukio ambapo ameagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha ghorofa hilo kuporomoka na pia kujiridhisha kama ujenzi ulifuata sheria na taratibu za ujenzi huku akitoa rai kwa Wananchi wote wanaojiandaa na ujenzi kupata vibali kabla ya kuanza kwa ujenzi ikiwemo kibali kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuepusha ajali zinazoepukika.

Kwa upande wake Afisa Zimamoto Wilaya ya Kigamboni , Mkaguzi Innocent Kirway Ingbertus amesema kwamba ghorofa liliporomoka wakati Mafundi wengine wakiwa juu na wengine chini hivyo kupelekea kufunikwa na mmoja ambaye alikuwa eneo hatarishi lenye shimo alifunikwa na zege na kufariki "Mkandarasi wa ujenzi aliondoka eneo la tukio na hajarudi hadi sasa, Mmiliki wa jengo pia hajafika eneo la tukio."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live