Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gharama ujenzi wa hospitali zamshtua kiongozi wa Mwenge

6f688ede9fa30d54a9732c82cf3f7dc4.jpeg Gharama ujenzi wa hospitali zamshtua kiongozi wa Mwenge

Sun, 18 Jul 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Josephine Mwampashi amekataa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tabora, baada ya kutoridhishwa na gharama zilizotumika katika ujenzi huo.

Kutokana na hali hiyo, amemwagiza Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa kufanya uchunguza wa kina wa gharama zote zilitumika katika mradi huo na kutoa taarifa haraka.

Alichukua hatua hiyo jana wakati Mwenge wa Uhuru ulipofika kukagua mradi huo na kubainiupungufu mwingi. Alisema licha ya mradi huo kupatiwa Sh milioni 140 za awali na baadaye Sh milioni 500 na kuongezewa Sh bilioni moja, lakini kazi iliyofanyika hailingani na kiasi kilichotumika.

“Sijaridhishwa na thamani ya fedha zilizotumika na kazi iliyotekelezwa. Watendaji wamekuwa wazembe kutunza fedha na kusimamia miradi ya serikali hali inayosababisha kukwamisha miradi ya wananchi.”

“Takukuru yuko wapi? njoo hapa, chukua hizi nyaraka zote kazichunguze na kutoa majibu haraka ili kujua hizi Sh milioni 140 walizopewa mwaka 2013/2014, Sh milioni 500, Sh milioni 166 na Sh bilioni moja walizopewa juzi juzi zimetumikaje ili tuchukue hatua,” alisema.

Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka alimpongeza kiongozi huyo wa mbio za Mwenge kwa kuchukua hatua hiyo ili Rais asikie kilio cha wakazi wa Tabora ambao wanahitaji kupata huduma ya hospitali hiyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz