Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gekul aitwa mahakamani

Gekul Awataka Wanasheria Kuwasaidia Wananchi Wenye Matatizo Pauline Gekul, aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Sun, 28 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama Kuu Tanzania Masjala ndogo ya Manyara imetoa wito kwa aliyekuwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria na  Mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul (CCM) kufika mahakamani hapo tarehe 18 Machi 2024. 

Wito huo unatokana na rufaa iliyokatwa na Hashim Ally anayewakilishwa na Wakili wake Peter Madeleka kwa kutoridhika na nia ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka nchini (DPP) ya kutoendelea na shauri hilo.

Gekul anatakiwa kufika mahakamani hapo  kwa ajili ya rufaa hiyo namba 577 ya mwaka 2024.

Tarehe 27 Desemba mwaka jana DPP aliwasilisha nia yake  ya kutoendelea na shauri namba 179 la mwaka 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Babati.

Hashimu alimshtaki Gekul kwa kosa moja la shambulio na kumsababishia madhara mwilini chini ya kifungo cha 241 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.

Gekul na Wenzake ambao hawakuwa mahakamami tarehe 11 Novemba mwaka jana walidaiwa kumweka kizuizini Hashimu huku wakimtisha na silaha ya moto  na kumvua nguo zake na kumlazimisha kukalia chupa ya soda ili iingie njia ya haja kubwa.

Kesi hiyo ilifunguliwa chini ya kifungu cha 128 (2) na (4) cha  sheria mwenendo wa makosa ya jinai (CPA).

Wakati huo huo Abdul Nondo Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa Chama cha ACTWazalendo tarehe 27 Novemba 2023 alimuandikia Barua Kamishna  wa Sekretariati ya Maadili ya Viongozi wa umma juu ya tuhuma za Gekul na kutaka achunguzwe.

Nondo alitumia fursa ya sheria namba 398 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2020) kifungu cha 25(1) kinachotoa fursa kwa mtu yeyote kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya kiongozi wa Umma juu ya uvunjifu wa sheria ya Maadili.

Nondo aliandika kwenye barua yake kuwa Gekul alikiuka sheria namba 398 kifungu cha 6(1)(a)  na 6(1)(b)(i)  ambavyo   vinahitaji viongozi wa umma kutenda majukumu yao ya kiofisi hata majukumu binafsi kwa kuzingatia Maadili,uaminifu,huruma na uadilifu.

Nondo alijibiwa kuwa malalamiko hayo yapo mbele ya vyombo vya haki hivyo chombo hicho kitakaa chonjo kuvipisha vyombo hivyo kufanya kazi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live