Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gari lililobeba mafuta ya Petroli lalipuka Mbeya, lajeruhi wawili

90700 Pic+moto Gari lililobeba mafuta ya Petroli lalipuka Mbeya, lajeruhi wawili

Fri, 3 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbeya. Gari lililobeba mafuta aina ya Petroli kutoka jijini Dar es Salam nchini Tanzania kwenda Zambia limelipuka na kujeruhi watu wawili pamoja na kuharibu gari la zimamoto katika eneo la Meta- Igurusi katika barabara kuu ya Mbeya/Njombe mkoani Mbeya.

Akizungumza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema gari lenye namba za usajili T956 DRT/ T886 DRV likiendeshwa na Issa Yusuph (35) lilipata hitilafu ya kiufundi Januari Mosi,2020, gari hilo lililipuka katika harakati za kufaulisha mafuta hayo siku iliyofuata (Jana).

“Chanzo cha ajali ni mlipuko uliotokea kwenye mashine ya kufaulishia mafuta aina ya ‘water pump’ majeruhi wamekimbizwa kituo cha afya Igurusi kwa matibabu,” amesema.

Matei amesema ajali hiyo imejeruhi watu wawili ambao ni Julius Daudi (30) na Stanford Mwakyusa (35) wote wakazi waIgurusi wilayani Mbarali.

Katika harakati za uokozi gari lenye namba za usajili SM 4633 mali ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji liliharibiwa na moto huo huku gari lililokuwa likihamishiwa mafuta lenye namba T 844 AWJ likiungua pia.

Chanzo: mwananchi.co.tz