Fri, 12 Jul 2019
Chanzo: mwananchi.co.tz
Mwanza. Jaji mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, Sam Rumanyika amezindua gari maalumu la Mahakama inayotembea litakaloweza kusaidia usikilizwaji wa mashauri katika Mkoa wa Mwanza.
Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 12, 2019 katika hafla inayoendelea eneo la viwanja vya Mahakama Kuu jijini Mwanza.
Jaji Rumanyika amesema gari hilo litaanza kutoa hudumia kata za Buswelu, Igoma na Buhongwa lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za mahakama, kufungua mashauri, wananchi kupata tarehe za mwendelezo wa kesi na kupata nakala za hukumu katika kipindi kifupi kisichozidi wiki moja.
Chanzo: mwananchi.co.tz