Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gambo aitaka Tarura kuwajibika

Gambo aitaka Tarura kuwajibika

Sat, 9 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura) Mkoani Arusha, wametakiwa kutekeleza miradi ya barabara kwa wakati huku watendaji wa halmashauri wakitakiwa kutoingilia majukumu ya Tarura.

Mkuu wa mkoa Arusha,Mrisho Gambo, Akizungumza wakati wa utiaji wa saini mikataba 28 ya ujenzi wa miradi 38 ya barabara katika halmashauri saba za mkoani Arusha, aliwataka Tarura kusimamia miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati.

Gambo amesema barabara ya urefu kilomita 70.23 za  kiwango cha lami pamoja na kiwango cha changarawe zitajengwa kwa gharama ya zaidi Sh5.85 bilioni.

Amesema Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya miundombinu ya barabara lakini baadhi haikamiliki kwa wakati.

"Wapo baadhi ya wakandarasi wanaotekeleza majukumu yao kwa usahihi na kwawakati lakini kuna wengine hawafahamu majukumu yao,"amesema.

Amesema ili kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo kama ilivyopangwa, ni vizuri wakandarasi wakashirikiana na Tarura kwa yale maeneo  yenye changamoto ili kuongeza nguvu ya utekelezaji wake.

Gambo pia alimwagiza Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega kuziandikia barua halmashauri zote mkoani Arusha kuacha kuingilia majukumu ya Tarura.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqaro amesema, wilaya hiyo ilikuwa na changamoto ya kusuasua kwa miradi ya barabara.

"Kuna baadhi ya wakandarasi wamekuwa wakisuasua kukamilisha miradi kwa wakati na kuleta usumbufu wa kurudia kwa matengenezo mengine," amesema.

Daqaro amesema kuna baadhi ya wakandarasi hawaheshimu sheria za kazi na wanawanyima haki wafanyakazi wao.

Mwishooo.

Chanzo: mwananchi.co.tz