Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Gambo aahidi neema ya umeme, maji safi Arusha

15542 Pic+gambo TanzaniaWeb

Tue, 4 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameahidi wakazi wa jiji la Arusha kuwa tatizo la umeme na kutopatikana maji safi katika jiji hilo, litabaki historia siku chache zijazo.

Akizungumza katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi wa jiji hilo, akiwa katika kata ya Olasiti, Gambo alisema kero kubwa katika jiji la Arusha ni kupatikana maji ya kutosha na umeme.

"Tayari tuna mikakati mikubwa ya kutatua matatizo haya, serikali imetoa fedha za miradi mikubwa ya maji na kuboresha usambazaji wa umeme na tuna uhakika siku si nyingi matatizo haya yatabaki historia," alisema.

Gambo amesema Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Makame Mbarawa alikuja Arusha na kushuhudia utiaji saini wa miradi ya maji na hivi karibuni atakuja Waziri wa Nishati, Medard Kalemani kutatua kero.

"Waziri Kalamani atakuja mkoani Arusha tarehe 5 mwezi huu na tutafanya ziara ya mtaa kwa mtaa kuhakikisha wanashughulikia kero ya nishati mkoani hapa," alisema.

Katika ziara hiyo, Gambo na viongozi wa taasisi za serikali na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Arusha wamekuwa wakijibu kero mbalimbali za wananchi.

Chanzo: mwananchi.co.tz