Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML) umetoa madawati elfu 8 yenye thamani ya shilingi Milioni 750 yatakayotumika kwenye shule mbalimbali wilayani ya Geita.
Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Terry Strong amesema kwa awamu ya kwanza wanakabidhi madawati elfu tatu ikiwa ni msaada kwa jamii kupitia fedha za uwajibikaji wa kampuni kwa Jamii.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema kwa mwaka huu wa fedha Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 9.7 kwa ajili ya mradi wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za msingi ( BOOST) ambapo wadau wa maendeleo wametakiwa kujitokeza kuisaidia Serikali katika kufanikisha mradi huo.
Afisa Elimu wa mkoa wa Geita, Anthony Mtweve amesema madawati hayo yatapunguza uhaba wa madawati kwa asilimia 42 wilayani Geita.