Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

GEUWASA yavunja mkataba na mkandarasi mradi wa maji

Majimji GEUWASA yavunja mkataba na mkandarasi mradi wa maji

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA) imevunja Mkataba wa Mradi wa ujenzi wa Maji wa Bung’wangoko uliopo kata ya Kasamwa wilayani Geita kwa kutoridhishwa na utendaji makandarasi aliyekuwa anatekeleza mradi.

Uamuzi huo umetolewa Meneja wa GEUWASA Mhandisi Frank Changawa baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa mradi huo uliofikia asilimia 15 pekee mpaka sasa.

Mradi wa maji ya Bung’wangoko ulikuwa unatekelezwa na mkandarasi Kelogi Construction kwa gharama ya Shilingi milioni 569 ambapo ujenzi wake ulianza Machi 7, 2023 na ulitarajiwa kumalizika Augusti 30, 2023.

Mhandisi Chang’awa amesema baada ya kutokamilika mkandarasi aliongezewa muda lakini cha kushangaza mpaka hadi Oktoba 25 2023 mradi ulikuwa Asilimia 15 na ndipo waliamua kuvunja mkataba huo.

"Niwakaikishie wananchi wa Bung’wangoko na maeneo jirani ambao ni wanufaika wa mradi tumevunja mkataba huu kwa haraka sana tunakwenda kumpa kazi mwingine Ili dhima hii ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itimie.

"Nakwenda kuomba kibali wizara ya maji Ili mradi huu ufanyike kwa njia ya force account ( mapato ya ndani) na mradi ukamilike kwa kasi.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live