Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Fuvu la binadamu lakutwa nje ya nyumba Rukwa

0ada63606ba96336939e692d300f12cc Fuvu la binadamu

Wed, 4 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkoani Rukwa katika kijiji cha Mtakuja pembezoni mwa ziwa Tanganyika wilaya ya Nkasi kimepatikana kichwa cha binadamu kimewekwa eneo la makazi ya watu. Mtaalamu wa Afya amehakikisha kuwa kichwa hicho ni cha binadamu aliezikwa siku za karibuni maeneo hayo.

RPC wa mkoa wa Rukwa William Mwapangale alithibitisha kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 25 July mwaka huu katika kijiji cha mtakuja wilaya ya Nyasi.

Alieleza kuwa kichwa cha binadamu huyo kilitelekezwa mbele ya nyumba ya Bi. Theresia Nyanyaga 75, mama Raymond anaeishi na mwanae mmoja Wa kike bi Reginal Raymond.

Mapema Asubuhi tarehe 25july mwaka huu siku ya tukio hilo Bi.Reginal Raymond alikwenda kujisaidia haja ndogO njee akakutana na harufu mbaya sana ndipo alipenda kumwambia mama yake na kwenda kutoa taarifa kwenye serikali ya mtaa na polisi , Alisema RPC.

Mwenyeketi wa kijji cha Mtakuja Bwana.Bernard Emmanuel aliongozana na vyombo vya usalama kwenye eneo la tukio ambapo mapolisi walibaini kihwa hicho kilinyofolewa kwenye mwili wa marehemu.

Mwili huo ulifukuliwa na kunyofolewa kichwa ,polisi wawewashikilia watu watatu kwa tuhuma yakuhusika kwenye kitedo hicho cha unyama alisema RPC.

Baada ya wataalamu wa afya kufanya uchunguzi kichwa cha binadamu huyo kilirudishwa kwenye kaburi lake. hata hivyo RPC alisema," watuhumiwa watatu nanashituiwa kuhusika watafikishwa mahakamani".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live